Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yataka nchi zitathmini hatua zilizopiga kupambana na ukimwi

UNAIDS yataka nchi zitathmini hatua zilizopiga kupambana na ukimwi

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wasuala ya ukimwi limetoa wito wa juhudi za kimataifa kurejea dhamira ya kuzisaidia nchi kufikia malengo ya kimataifa ya kuzuia virusi vya HIV, matibabu, huduma na msaada.

Nchi zinatakiwa kuchukua msiamamo wa mpango wa wazi na utakaozileta pamoja serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya jumuiya za kijamii, mtandao wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na makundi ya kijamii ili kutathmini maendeleo yaliyopigwa katika kufikia malengo ya kitaifa ya mapambano dhidi ya ukimwi.

UNAIDS itazisaidia nchi hizi na vyomvo mbalimbali husika ili waweze kutathmini maendeleo waliyopiga. Wito huu umetolewa nchini Botswana na mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe aliyeko ziarani kusini mwa Afrika.