Mkuu wa mabadiliko ya hali ya hewa wa UM kujiuzulu

18 Februari 2010

Mkuu wa masuala ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa Yvo de Boer leo ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake kama katibu mkuu wa mpango wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa kuanzia tarehe mosi July mwaka huu wa 2010.

Bwana de Boer ambaye amefanya kazi na mpango huo tangu mwaka 2006 amesema kufanya kazi katika kitengo hicho na wenzie na kuunga mkono majadiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa imekuwa ni uzoefu mzuri na wa mafanikio kwake.

Licha ya kwamba wafanyakazi wenzie wamemuelezea kuwa ni mtu mwenye ushirikiano na mchapa kazi lakini kama anavyosema Eric Hall aliyefanya kazi na bwana de Boer uamuzi wa kuondoka wa bwana de Boer haukuwa rahisi

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter