Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Washukiwa wawili wa shambulio dhidi ya UNAMID wamekamatwa

Washukiwa wawili wa shambulio dhidi ya UNAMID wamekamatwa

Mkuu wa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID, Ibrahim Gambari leo amesema washukiwa wawili wa shambulio la karibuni dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya UNAMID wamekamatwa.

Bwana Gambari amewaambia waandishi wa habari taarifa hizo kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Mutrif Siddiq mjini Khartoum.

Amesema haya ni maendeleo mazuri ambayo yatasaidia kurejesha hali ya utulivu Darfur na pia kuvisaidia vikosi vya UNAMID kutekeleza wajibu wake.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuwafikisha watu hawa mahakamani na wasomewe hukumu pamoja kwani itatoa ujumbe kwamba kuwashambulia askari wa kulinda amani ni kitu kisichovumilika.