Mkataba wa kupinga mabomu mtawanyiko kuanza kutekelezwa August mosi

17 Februari 2010

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua kubwa ya ajenda ya upokonyaji silaha wa kimataifa, wakati Umoja wa Mataifa ulipopokea mswaada wa kuridhia mkataba dhidi ya mabomu mtawanyiko.

Taarifa kutoka kwa msemaji wa Umoja wa Mataifa imebaini kwamba kwa hatua hii mkataba utaanza kufanya kazi tarehe mosi ya mwezi August mwaka huu .

Mkataba huo utaanza kutekelezwa miaka miwili baada ya ulimwengu kuonyesha nia ya pamoja ya kupambana na athari za silaha hizo ambazo wakati na baada ya vita zimekuwa zikiendelea kukatili maisha ya watu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud