Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yamulika usawa wa kijinsia

FAO yamulika usawa wa kijinsia

Mfumo mpya wa kuhifadhi takwimu uliozinduliwa na shirika la kimataifa la chakula na kilimo FAO, unalipiga darubini swala la usawa wa kijinsia ambalo limekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo vijijini, hasa tofauti baina ya wanawake na wanaume katika suala la kumiliki ardhi.

Mfumo huo wa takwimu kwa masuala ya usawa wa kijinsia na haki ya umilikaji ardhi uliozinduliwa kwa kushirikisha, kitengo cha taifa cha takwimu, vyuo vikuu, mashirika ya jumuiya za kiraia na vyanzo vingine kote duniani, unatoa taarifa mpya za jinsi wanawake na wanaume katika nchi 78 wanavyotofautiana katika haki za kisheria na uwezo wa kumiliki ardhi.

Katika nchi nyingi duniani wanawake wako nyuma katika umilikaji wa ardhi ya kilimo na mapato yatokanayo na ardhi, ingawa wao ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na ndio wanaotunza familia.