Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa kibinadamu kuwafaidi Waafghani milioni saba

Msaada wa kibinadamu kuwafaidi Waafghani milioni saba

Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA na serikali ya Afghanistan leo wamewasilisha rasmi mpango wa 2010 wa kuufanyia kazi katika masuala ya kibinadamu mjini Kabul.

Mpango huo una lengo wa kuimarisha uwezekano wa mpango wa wakati wote wa kuisaidia nchini ya Afghanistan amesema Robert Watkins naibu mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan.

OCHA inasema ongezeko la hofu ya usalama, maporomoko, matetemeko ya ardhi, ukame na mafuriko vimewaacha Waafghanistan wengi katika hali mbaya na wanahitaji msaada wa haraka.