Skip to main content

Wanajeshi saba wa UNAMID wajeruhiwa Darfur

Wanajeshi saba wa UNAMID wajeruhiwa Darfur

Askari saba wa kikosi cha polisi cha jeshi la kulinda amani la Umoja wa Maifa na Umoja wa Afrika Darfur UNAMID wamejeruhiwa nje kidogo ya eneo la Nyala kusini mwa Darfur nchini Sudan.

Askari hao wa kulinda amani kutoka Pakistan walikuwa katika msururu wa magari saba ya UNAMID wakirejea kwenye kituo chao cha Nyala waliposhambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Tukio hilo lilitokea jana karibu na eneo la Sakali , lililopo kilometa mbili kutoka kambi ya El-sherif ya wakimbizi wa ndani kusini mwa Nyala.