Na wakati huohuo idara ya Marekani inayohusiaka na masuala ya kufuatilia na kukabiliana moja kwa moja na usafirishaji haramu wa watu GTIP,italipa ufadhili mradi wa shrika la kimataifa linalohusiaka na masuala ya uhamiaji IOM.
Msaada huo ni ili kuisaidia Sri Lanka kuanzisha mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa wqatu , kuwatambua na kuzichukulia sheria kesi zote za usafirishaji haramu wa watu. Pia kuwalinda waathirika wa vitendo hivyo na kuimarisha mfumo wa serikali wa takwimu za usafirishaji haramu wa watu.
Mradi huo utakaogharimu dola 300,000 utatoa pia mafunzo kwa wanaohusika na sheria ,maafisa wa serikali na itatoa msaada wa kiufundi kwa wafanyakazi wa serikali wa kuzuia usafirishaji haramu ,ili kuwasaidia kutekeleza mkakati huo wa kitaifa.