Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon atangaza jopo la kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa

Ban Ki-moon atangaza jopo la kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa

Viongozi wa Uingereza na Ethiopia wataongoza jopo jipya la ngazi ya juu lililozinduliwa leo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ,lenye lengo la kukusanya fedha ili kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkataba ulioafikiwa mwezi Desemba mjini Copenhagen Denmark kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa, yalikuwa ni mwanzo wa hatua za haraka za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na muongozo wa majadiliano ya hatua za muda mrefu, ambapo waliahidi kukusanya dola bilioni 100 kila mwaka ifikapo mwaka 2020.

Kwa kufanya hivyo bwana Ban amesema kutakuwa na uwiano baina ya nchi zinzoendelea na zile zilizokwisha endelea . Katika jopo hili jipya la ushauri wa masuala ya fedha za kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa ambalo linaongozzwa na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi na waziri mkuu wa Uingereza Gordon.