Skip to main content

Ingawa hatua umepigwa kuisaidia Haiti jitihada zaidi zahitajika

Ingawa hatua umepigwa kuisaidia Haiti jitihada zaidi zahitajika

Ni mwezi mmoja sasa tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti lililosababisha vifo vya watu wengi na uharibifu mkubwa.

 OCHA inasema kwa ujumla hali ya usalama imeimarika kwa msaada wa polisi wa Haiti,Umoja wa Mataifa , serikali ya Marekani na jeshi la Canada ambalo linatoa ulinzi.

Licha ya hatua hiyo iliyopigwa hata hivyo ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu na kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya wakimbizi wamesema wakati msaada wa kimataifa kusaidia kadhia ya Haiti unaendelea vizuri , bado msaada na hudumu muhimu hazijaifikia idadi kuwa ya watu walioathirika. Na wengi wanakosa huduma muhimu kama chakula, malazi, maji na huduma za afya. Melisa Fleming ni msemaji wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR