Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa upokonyaji silaha wamalizika bila mafanikio

Mkutano wa upokonyaji silaha wamalizika bila mafanikio

Maendeleo katika mkutano wa upokonyaji silaha mwaka huu yamekuwa mabaya sana, kwani mkutano huo umeshindwa hata kufikia jambo la kulifanyia kazi, amesema mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Sergei Ordzhonikidze katika hafla ya kufunga mkutano huo mapema leo.

Amesema kwa muda wa wiki nne za mkutano huo na matumizi makubwa ya bajeti ya Umoja wa Mataifa kuendesha mkutano, hakuna matunda yoyote yaliyopatikana ni sifuri, hivyo amesema uvumilivu wake kwa mahusiano ya kimataifa sasa unaanza kupungua.

Amehitimisha kwa kusema kwamba hadi hapo mkutano huo utakapotanabahi hali ya sasa ya uhusiano wa kimataifa basi hauna msingi wowote, na kwa niaba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea kusikitishwa kwake na juhudi ndogo zilizofanyika na hivyo kutofanikisha nia ya mkutano huo.