Wataalamu wa UM wanatumai kukutana na Aung San Suu Kyi

Wataalamu wa UM wanatumai kukutana na Aung San Suu Kyi

Wataalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Myanmar wanasema wanatumai kukutana na kiongozi wa upinzani nchini humo Bi Aung San Su Kyi wakati wa ziara yao nchini humo wiki ijayo.

Tomas Quintana ambaye atakuwa nchini Myanmar kwa wiki moja kuanzia Jumatatu ijayo kwa mwaliko wa serikali pia anatarajia kukutana na viongozi wengine wa kisiasa katika safari yake ya tatu nchini humo.Anasema anatumai ombi lake kwa serikali la kukutana na Aung San Suu Kyi litakubaliwa safari hii, akisisitiza umuhimu wa kukutana na viongozi wa kisiasa watakaoshiriki uchaguzi wa mwaka huu.Wataalamu wanasema mwaka huu wa 2010 ni muhimu sana kwa watu wa Myanmar hasa kwa kuwa serikali itafanya uchaguzi baada ya miaka 20.

Aung Suu Kyi chama chake cha National League for Democracy kilishinda uchaguzi mwaka 1990 na akachaguliwa kuwa waziri mkuu, lakini amekuwepo katika kifungo cha nyumbani kwa karibu miaka 14 sasa.