Skip to main content

UM na MTV washiriki vita dhidi ya ukimwi Kenya

UM na MTV washiriki vita dhidi ya ukimwi Kenya

Umoja wa Mataifa na MTV wako katika mkakati wa kuwafikia vijana nchini Kenya na kuwaelimisha kuwa virusi vya ukimwi sio hukumu ya kifo kwa kutumia tamthilia mpya ya televisheni yenye sehemu tatu inagusia maisha na mapenzi ya kundi la marafiki mjini Nairobi.

Mchezo huo wa kuigiza uliopewa jina la SHUGA ni wa kusisimua lakini unatoa mafunzo, kwa vijana kuhusu hatari inayowakabili ya kupata.

Kinara katika tamthilia hiyo ni binti Lupita Nyon'go ambaye jina la mchezo anajulikana kama Ayira. Nafasi yake katika mchezo huo ni mwanafunzi wa chuo ambaye anajikuta njia panda, upande akiwa na mpenzi kijana mwenzie, na upande wa pili ana mzee ambaye ni suga dady. Nia ni kuonyesha jinsi gani tabia ikiwa ni pamoja na kuwa na wapenzi wengi wakushirikiana nao kingono, ukandamizaji na matumizi ya pombe vinavyoweza kuchangia ongezeko la maambukizi ya ukimwi .

Ujumbe kuhusu kujikinga na ukimwi ni muhimu saana hususani Mashariki na Kusini mwa Afrika ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ndio kitovu cha waathirika wa ugonjwa huo na hasa wasichana.

Takwimu za UNICEF, UNAIDS na shirika la afya duniani WHO zinaonesha kati ya watu karibu milioni 40 walioko nchini Kenya watu milioni mbili wanaishi na virusi vya ukimwi.

Hata hivyo UNICEF inakiri kwamba michezo maarufu pekee kama Shuga haitotokomeza gonjwa la ukimwi, lakini itasaidia kupiga vita unyanyapaa ambao unawakabili waathirika wengi.