Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa wito wa msaada kwa wakimbizi wa Pakistan

IOM yatoa wito wa msaada kwa wakimbizi wa Pakistan

IOM imetoa wito wa msaada wa dola milioni 16 ili kuwasaidia wakimbizi wa ndani kaskazini magharibi mwa Pakistan.

IOM inasema fedha hizo zitatumika kusaidia makazi ya dharura kwa familia zinazorejea makwao na pia kuijenga upya miundombinu ya eneo hilo iliyoharibiwa vibaya na operesheni za kijeshi.

Msaada pia utajumuisha kutoa mafunzo ya usalama kwa mashirika yanayotoa msaada katika maeneo yaliyoathirika na vita, pia kampeni za kuwapasha habari watu kwa niaba ya serikali na makundi ya misaada ya kibinadamu.

Kuna watu laki nane walioachwa bila makazi kaskazini magharibi mwa Pakistan na IOM inahitaji dola hizo milioni 16 ili kuendelea kufanya kazi yake hasa katika eneo la Fata .