Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaisaidia vifaa wizara ya afya ya Zimbabwe

IOM yaisaidia vifaa wizara ya afya ya Zimbabwe

Shirika la kimataifa linaloshughulikia masuala ya uhamiaji IOM limeikabidhi wizara ya afya na maendeleo ya watoto ya Zimbabwe ,vifaa vya mawasiliano ya redio, katika juhudi za kuiwezesha kuripoti milipuko ya magonjwa na kuchukua hatua zinazostahili katika vituo vya afya vya vijijini hasa katika maeneo ya mpakani.

Msaada huo ambao umefadhiliwa na kitengo cha tume ya umoja wa Ulaya cha masuala ya misaada ya kibinadamu (ECHO) ni sehemu ya mradi mkubwa wa kuangalia hali ya dharura ya ugonjwa wa kipindupindu na kuidhibiti katika maeneo ya mpakani kama Hurungwe, Mbire, Mlima Darwin, Mudzi, Mutare, Chipinge, Chimanimani na Chiredzi.

Kila wilaya itapata vifaa vya mawasiliano ili kuondoa pingamizi ya mawasiliano iliyokuwepo baiana ya vituo vya afya vya vijijini na hospitali za wilaya. Chis Lom kutoka IOM anafafanua faiada ya vifaa hivyo