IAEA imepokea barua kutoka Iran kuhusu uranium

IAEA imepokea barua kutoka Iran kuhusu uranium

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA limethibitisha kwamba limepokea barua kutoka Iran ikielezea nia ya nchi hiyo ya kuanza kuzalisha uranium kwa kiwango cha hadi asilimia 20%.

Taarifa hiyo haikutoa tarehe kamili ya kuanza uzalishaji lakini kwa mujibu wa Tehran huenda ikaanza mapema kuanzia leo Jumanne.

Wakati huohuo mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Maita Ban Ki-moon kwa Jamhuri ya watu wa Korea ,amewasili leo mjini Pyongyan. Alipowasili kwenye uwanja wa ndege mjini humo Lynn Pascoe anayewakilisha Umoja wa Mataifa kwa masuala ya kisiasa ameliambia shirika la habari ya Xinhua kwamba maafisa wa Jamuhuri ya Korea watajadiliana naye njia za kuimarisha uhusiano baina ya Umoja wa Mataifa na Jamhuri ya Korea.