Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa katika kuisaidia Haiti

Hatua zimepigwa katika kuisaidia Haiti

Shirika la afya duniani WHO linasema ripoti za watu waliojeruhiwa vibaya katika tetemeko la ardhi Haiti ambazo zilikuwa zaidi ya asilimia 20% sasa zimeanza kupungua, lakini bado watu hao wanawakilisha asilimia 10 ya wagonjwa wote.

Shirika hilo pia limesema hakuna ongezeko la magonjwa ya kuambukiza ambayo yameripotiwa.

Nayo OCHA kwa upande wake inasema zaidi ya watu milioni 1.2 wamepatiwa makazi ya muda na wengine laki 467,701 wameondoka Port-au-Prince kupata makazi sehemu nyingine.

Utoaji wa vifaa vya malazi bado ni jambo linalopewa umuhimu mkubwa katika maeneo yote yaliyoathirika , ndege za misaada zinahamisha watu na kuwapeleka sehemu mbalimbali za Haiti .Bi Elizabeth Byrs wa OCHA anasema umuhimu mkubwa unatolewa kwa kuwapa watu malazi.