Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID yasifu kuachiliwa kwa mfanyakazi wa misaada

UNAMID yasifu kuachiliwa kwa mfanyakazi wa misaada

Jeshi la kulinda amani la ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID nchini Chad ,limesema limepokea kwa furaha taarifa za kuachiliwa bwana Laurent Maurice Mfaransa na mfanyakazi wa shirika la misaada la kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu, baada ya kushikiliwa karibu miezi mitatu.

Bwana Maurice alitekwa na watu wenye silaha wasiojulikana tarehe 9 Novemba mwaka jana mashariki mwa Chad, alipokuwa katika kazi ya kutathmini hali ya mavuno nchini humo kilometa 10 kutoka kwenye mpaka na Sudan.

Bwana Maurice aliachiliwa siku ya Jumamosi na akapelekwa moja kwa moja mjini Khartoum ambako amepatiwa matibabu.