Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama waimarisha kwa wakimbizi wa ndani Congo DRC

Usalama waimarisha kwa wakimbizi wa ndani Congo DRC

Hali ya usalama kwa wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni mbaya, wakati wengi wakiendelea kutekwa na makundi ya watu wenye silaha ambayo yanawashinikiza kufanya kazi ngumu katika maeneo mengi ya jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Hali hii inaendelea licha ya serikali kuongeza ulinzi na kuimarisha usalama. Wanaume wengi katika kambi hizo wamearifiwa kushinda nje ya kambi wakihofia kutekwa. Hata hivyo habari zinaema utekaji mwingi unafanyika nyakati za usiku. Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA, mji wa Rutshuru ambao una wakimbizi wa ndani karibu 129,000 ndio ulioathirika zaidi.