Skip to main content

Kampeni ya chanjo ya dharura yaanza Haiti

Kampeni ya chanjo ya dharura yaanza Haiti

Kampeni ya chanjo ya kuwakinga na maradhi mbalimbali watu walioathirika na tetemeko nchini Haiti imeanza.

Watu takribani 140,000 watanufaika na kampeni hiyo ya chanjo ya dharura ambayo inaanza leo. Chanjo hiyo imepigiwa upatu na wizara ya afya ya Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la Kimarekani la masuala ya afya (PAHO)

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu , ndio mshirika mkubwa katika kampeni hiyo, na inawachagiza watu wapatao 100 wengi wao wakiwa kutoka shirika la msalaba mwekundu la Haiti, kujitolea kuhamasisha watu. Shirikisho hilo linatarajia aslimia 80% ya watu kupata chanjo.

Kampeni hiyo kwa sasa itajikita Port -au -Prince kwasababu watu wengi wako kwenye hatari ya kupata maradhi kuliko kwengineko. Chanjo kwa sasa inafanyika kwenye uwanja wa mpira kama anavyoeleza Dr Robin Nandy mshauri wa masuala ya afya wa UNICEF.