UNICEF: Ongezeko la ukeketaji latia hofu

5 Februari 2010

UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO wameelezea wasiwasi juu ya kuongezeka kwa wahudumu wa afya wanaoendesha vitendo vya ukeketaji. Inakadiriwa kuwa wanawake milioni 120 hadi 140 wamekeketwa na wasichana milioni 3 bado wako kwenye hatari ya kukeketwa kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji. Shirika la afya duniani WHO linasema takribani asilimia 18% ya ukeketaji huo unafanywa na wahudumu wa afya hali ambayo haitakiwi kuendelea . Nchi ambazo wahudumu wa afya wanatekeleza vitendo hivyo ni Misri, Sudan, Kenya , Yemen na Guinea Konakry.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter