Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada yaanza kuwasili kama inavyotakiwa Haiti

Misaada yaanza kuwasili kama inavyotakiwa Haiti

Ugawaji wa misaada ya dharura unaendelea bila mushkeli wowote hivi sasa nchini Haiti. Lakini bado kunahitajika kuimarisha usambazaji wa vifaa vya usafi. Vyoo vinavyohamishika elfu 25 vinahitajika ili kuwahudumia watu laki tano walioko Port au Prince.

WFP imefanikiwa kupeleka msaada wa chakula kwa watu milioni 1.6 katika maeneo ya Port au Prince na viunga vyake. Vituo 16 vya ugawaji chakula vimewawezesha watu laki sita na nusu kupata mgao wa chakula.

Mashirika ya misaada ya kibinadamu 55 hivi sasa y yako Haiti na yanatoa vifaa mbalimbali ikiwemo maturubai, kamba na vifaa vingine vya ujenzi kwa watu milioni 1.1 kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua. Na mwezi huu kutafanyika mkutano mjini Roma kujadili mipango ya kuendeleza upya sekta ya kilimo ya Haiti anasema Bi Emilia Casella wa WFP.