Skip to main content

Mkutano wa kimataifa kupigia chepuo ya amani ya Palestina na Israel kufanyika:

Mkutano wa kimataifa kupigia chepuo ya amani ya Palestina na Israel kufanyika:

Kamati inayoshughulikia masuala ya haki za watu wa Palestina na bunge la Mediteraniani wataandaa mkutano wa kimataifa kuunga mkono amani baina ya Israel na Palestina mjini Qawra Malta tarehe 12 na 13 mwezi huu.

Ajenda kuu ya mkutano huo itakuwa ni umuhimu wa haraka wa kupata suluhu ya kudumu ya masuala kama ya mipaka, Jerusalem, makazi, wakimbizi na maji. Pia kutoa nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu hali ya sasa ya mpango wa amani na kuchagiza mazungumzo miongoni mwa wahusika ya jinsi ya kuweka mazingira mazuri ya kisiasa yatakayosaidia kurejesha majadiliano ya amani ya kudumu. Mkutano huo pia utaangalia jinsi ya kuondoa tofauti baina ya pande husika na kujenga imani miongoni mwao.