Skip to main content

Watu zaidi ya milioni 12 wapatikana na saratani kila mwaka:

Watu zaidi ya milioni 12 wapatikana na saratani kila mwaka:

Leo ni siku ya kimataifa ya saratani, na mwaka huu juhudi zinaelekezwa katika kuzuia ugonjwa huo. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, kila mwaka watu zaidi ya milioni 12 wanapimwa na kukutwa na ugonjwa wa saratani.

WHO inasema saratani inaua watu wengi zaidi kuliko ukichanganya pamoja ukimwi, malaria na kifua kikuu. Lakini habari njema ni kwamba takribani aina mbili kati ya tano za saratani zinazuilika. Dr Andreas Ullrich wa kitengo cha kuzuia saratani cha WHO anafafanua ukubwa wa tatizo la saratani.