UNICEF:Watoto ni waathirika wakubwa katika majanga:

4 Februari 2010

Watoto ndio wanaoathirika sana duniani kutokana na sababu mbalimbali, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakati wa uzinduzi wa ripoti yake ya masuala ya kibinadamu kwa mwaka huu wa 2010.

Ripoti hiyo imebaini kwamba majanga yanapotokea kote duniani waathirika wakubwa ni watoto na wanawake, na wote wanahitaji msaada.

Kwa mujibu wa naibu mkurugenzi mkuu wa UNICEF Hilde F. Johnson mwaka wa 2009 majanga makubwa ya asili na yaliyosababishwa na binadamu ,yalilikumba eneo la kusini mwa Asia ,wakati hali ya dharura ikizikabili nchi za pembe ya Afrika, Afghanistan, Pakistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan.

Amesema, majanga hayo yanawaweka katika hatari ya kunyanyaswa na haki zao kukiukwa ,ikiwa ni pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kuuawa na kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter