Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa kufuta madeni yote ya Haiti:

Wito watolewa kufuta madeni yote ya Haiti:

Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu , Cephas Lumina leo Alhamisi ametoa wito wa kufutwa mara moja madeni ya Haiti inayodaiwa na wadeni mbalimbali na kuipa nchi hiyo fedha za msaada zisizo na masharti yoyote, na sio mkopo mpya.

Amesema kinachotakiwa hivi sasa ni kufuta madeni kama ambavyo UNCTAD na wengine wamesema hivi karibuni. Mtaalamu huyo ameupongeza uamuzi wa Paris club ambayo ni muungano wa nchi 19 wakopeshaji, ambao wamesema watafuta deni la dola milioni 214 wanazoidai Haiti. Hata hivyo ameonya kwamba uamuzi huo hautoshi kuirejesha nchi hiyo katika hali ya kawaida