Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wafanyika kwenye mtandao khusu masuala ya wanawake na vyombo vya habari

Mjadala wafanyika kwenye mtandao khusu masuala ya wanawake na vyombo vya habari

Umoja wa Maita umewaalika waandishi wa habari, wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wanafunzi na wanazuoni kushiriki mjadala unaofanyika kwenye mtandao kuhusu "Wanawake na vyombo vya habari."

Wanawake na vyombo vya habari ni moja ya mfululizo wa mijadala inayofanyika kwenye mtandao kuazimisha miaka 15, tangu kupitishwa azimio la Beijing la kuchukua hatua za kumkomboa mwanamke, ambalo ni matokeo ya mkutano wa kihistoria wa wanawake uliofanyika mjini Beijing mwaka 1995.

Uchambuzi wa yapi yaliyoafiikiwa tangu Beijing na mjadala wa hatua gani zaidi zichukuliwe katika mapendekezo ya miaka 15 iliyopita utafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York ,wakati wa kikao cha 54 cha tume ya UM kuhusu hali ya wanawake ,kuanzia tarehe mosi hadi 12 Machi mwaka huu.