Juhudi zinafanyika kumaliza ukatili wa kimapenzi

3 Februari 2010

Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha msaada wa kutafuta amani kimeamua kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ,ili kuzuia ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya migogoro na kutoa msaada unaohitajika kwa waathirika.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, kutokana na wito wa makundi ya kina mama, waathirika wa ubakaji na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S) ameanzisha mtandao wa mashirika hayo ujulikanao kama "Hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na ukatili wa kimapenzi katika migogoro 2008)

Mtandao huo utawajumuisha pamoja wataalamu wa masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulinda amani, HIV na ukimwi, na haki za binadamu , ili kusaidia kukomesha ubakaji, na uhalifu wa kimapenzi katika nchi zilizoko katika vita.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud