Skip to main content

Zaidi ya dola bilion 2 zimekusanywa kwa ajili ya kuisaidia Haiti

Zaidi ya dola bilion 2 zimekusanywa kwa ajili ya kuisaidia Haiti

Mkuu wa masuala ya ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa John Holmes, amesema zaidi ya dola bilioni 2 zimechangwa au kuahidiwa kwa ajili ya kuisaidia Haiti, na kwa sasa wito wa msaada huo umefikia asilimia 83.

Amesema hata hivyo bado kuna maeneo mengine ambayo hajafadhiliwa vya kutosha , kama elimu, kilimo , kuwarejesha watu katika maisha ya kawaida, lishe bora na usalama.

Bwana Holems ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva kuwa shughuli za misaada nchini Haiti zimekumbwa na matatizo na zinafanyika polepole, lakini hatua inapigwa.