ICRC yasema juhudi zaidi zatakiwa kuwalinda watoto Haiti

ICRC yasema juhudi zaidi zatakiwa kuwalinda watoto Haiti

Mshauri wa masuala ya kuwalinda watoto wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC Kristin Barstad amesema , tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni limewaathiri vibaya watoto hasa waliopoteza wazazi wao.

Amesema ICRC inashirikiana na mashirika mengine ili kupata suluhu muafaka ya kuwasaidia watoto wasio na watu wa kuwaangalia. Ameongeza kuwa ,"Wakati huu wakijaribu kuwapata ndugu wa watoto hao pia wanafanya kazi na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu nchini humo ili kupata matunzo ya watoto hao na kuhakikisha wanapata kila wanachohitaji.

ICRC na shirika la msalaba mwekundu la Haiti wanaweka msisitizo wa kuwapata watoto ambao wako peke yao , au walio na watu wa kuwaangalia ,ili kuwapa msaada wa kuwatafuta ndugu zao.