Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yatakiwa kuamua tena dhidi ya kesi inyomkabili Omar al-Bashir

ICC yatakiwa kuamua tena dhidi ya kesi inyomkabili Omar al-Bashir

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko mjini The Hague Uholanzi imeamriwa kuamua tena endapo Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir ni lazima akabiliwe na mashitaka ya ziada ya kutekeleza mauaji ya kimbari kwenye jimbo la Dafur.

Uamuzi huo umeafikiwa na majaji wa rufaa leo jumatano katika mahakama hiyo.

Majaji wamebadili uamuzi wao kwamba waendesha mashitaka hawakutoa ushahidi wa kutosha kuongeza mashitaka ya mauji ya kimbari kwenye kesi ya Rais Bashir, ambayo tayari yanajumuisha makosa saba ya ukatili dhidi ya binadamu, na uhalifu wa vita, ikiwemo mauji, unyanyasaji, na ubakaji.. Bi Sonia Robla ni mkuu wa idara ya habari ya ICC.