Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita vinavyoendelea Somalia vya wafanya raia zaidi kuvunga virago

Vita vinavyoendelea Somalia vya wafanya raia zaidi kuvunga virago

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema machafuko yaliyoongezeka mwezi wa Januari nchini Somalia , yamesababisha vifio vya mamia ya raia na uharibifu mkubwa.

Shirika hilo linasema mapigano baiana ya majeshi ya serikali ya mpito na makundi ya wanamgambo wanaodhibiti eneo la katikati mwa Somalia ,yamesababisha vifo vya raia 258. Hata hivyo mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kufanya shughuli zao nchini humo ili kuwasaidia raia ikiwemo WHO.

WHO inasema inashirikiana na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali nchini Somalia ili kukabiliana na maradhi mbalimbali hasa wakati huu ambako kuna dalili ya kusambaa kwa ugonjwa wa kuhara katika sehemu ya katikati na kusini mwa Somalia.

Machafuko haya ya karibuni yamewafanya maelfu ya raia kufungasha virago na kukimbia mji wa Moghadishu na viunga vyake. Hivi sasa kuna taarifa za mapigano kuzuka upya katika eneo la kati la Somalia na maelfu ya familia zimeacha bila makazi. Na wakati hayo yakiendelea ukame umelikumba eneo la mpakani mwa Ethiopia na Kenya ambako maradhi ya utapia mlo kwa watoto yamekithiri, na kuwaweka wakimbizi katika hali mbaya zaidi.