Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waasi wa Uganda wauwa raia 100 mashariki mwa Congo

Waasi wa Uganda wauwa raia 100 mashariki mwa Congo

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema watu 100 wameuawa na kundi la waasi wa Uganda , nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kipindi cha mwezi uliopita pekee.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na ofisi ya uratibu wa masuala ya kibinadamu (OCHA) kundi la Lord's Resistance Army (LRA) lilishambulia kijiji cha Mabanga kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tarehe 13 mwezi Januari.

Idadi kamili ya watu wote waliouawa na kundi la LRA hadi sasa tangu walipoanza uasi katika eneo hilo, bado haijajulikana lakini OCHA inasema kwa mwezi wa Desember 2009 zaidi ya watu 80 waliuaa. OCHA pia imeelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya makambi ya wakimbizi wa ndani.

Kwa upande wake majeshi ya serikali ya Congo yameshutumiwa kwa kuchukua misaada ya mshairika yasiyo ya kiserikali katika kambi ya Muhanga Kivu ya Kaskazini na hivyo kuvuruga shughuli za ugawaji wa misaada katika kambi hiyo.