Skip to main content

Mashirika ya kibinadamu yahofia hali ya Congo DRC

Mashirika ya kibinadamu yahofia hali ya Congo DRC

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayofanya kazi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , bado yanahofia hali ya ukiukaji mkubwa wa mara kwa mara wa sheria na haki za wakimbizi wa ndani walioko katika kambi nchini humo.

Tarehe 22 mwezi Januari , kulifanyika uvamizi katika kambi ya Nyange eneo la Masisi kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini, uvamizi huo unadaiwa kufanya na kundi la FDLR. Watu watatu wamearifiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.