Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahimizia msaada kwa mahitaji ya maendeleo Africa

Ban ahimizia msaada kwa mahitaji ya maendeleo Africa

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameahidi kuhamasisha msaada wa kukabiliana na changamoto zinazitishia amani na maendeleo barani Afrika, ikiwa ni pamoja na umasikini uliokithiri, masuala ya kiuchumi na kijamii na matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Afrika hapo jana bwana Ban amegusia mkutano wa Umoja wa Mataifa hapo mwezi September utakaojikita katika malengo ya milenia, kama kipimo cha kimataifa cha malengo waliyoafikiana ya kutokomeza umasikini na matatizo mengi ifikapo 2015.

Mkutano huo wa Septemver kuhusu malengo ya milenia utafanyika sambaba na ufunguzi wa mkutano mkuu ambapo viongozi kutoka nchi 192 wanachama wa umoja wa mataifa wanakutana kila mwaka katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.