Skip to main content

Wamarekani 10 washikiliwa kwa kuchukuwa watoto Haiti bila vibali

Wamarekani 10 washikiliwa kwa kuchukuwa watoto Haiti bila vibali

Wamishonari 10 kutoka kundi la Marekani lijulikanalo kama New Life Refuge walikamatwa kwenye mpaka Santo Domingo wakiwa na watoto 33 wa Kihatiti bila ya kuwa na vibali vya aina yoyote vya kuwachukua watoto hao, na wala ushahidi kuwa watoto hao ni yatima.

Ikulu ya Marekani jana jumapili imesema itarejea shughuli ya kuwahamisha watu waliojeruhiwa vibaya katika tetemeko la ardhi nchini Haiti kuwapeleka kwenye hospitali za nchini Marekani. Shughuli za misaada ya kibinadamu zilisitishwa siku tano zilizopita kufuatia malalamiko kutoka jimbo la Florida kuwa hospitali zake zimezidiwa na idadi ya wagonjwa.