Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti mpya unagundua idadi ya vifo kutokana na vita DRC ni juu sana

Utafiti mpya unagundua idadi ya vifo kutokana na vita DRC ni juu sana

Karibuni katika makala yetu ya wiki ambapo hii leo tutazungumzia mjadala ulozuka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na utafiti mpya unaoeleza kwamba idadi ya vifo milioni 5.4 kutokana na vita ni ya juu sana.

Imekuwa ikiripotiwa kwamba vita vya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vimekua vikiripotiwa vimesababisha karibu vifo vya watu milioni 5.4 vikiwa ni vita vilivyo sababisha maafa makubwa tagu vita vikuu vya dunia.

Idadi hiyo ya vifo vilivyotokea tangu 1998 inatokana na utafiti ulofanywa na kundi la huduma za dharura lenye makazi yake mjini New York International rescue committe IRC. Utafiti huo ulieleza kwamba idadi hiyo siyo ya vifo kutokana na vita moja kwa moja pekee bali pia ni pamoja na vile vinavyotokana na athari za vita ikiwa ni njaa na magonjwa.

Lakini siku ya Ijumatano matokeo ya utafiti mpya yanaeleza kwamba idadi ya vifo kutokana na vita vya Kongo inaweza kuwa ya chini zaidi ikiwa utaratibu unaostahiki unatumiwa. Mkurugenzi wa mradi wa utafiti wa katika Chuo Kikuu cha Simon Fraser huko Canada, Andrew Mack, anasema kundi lake limegundua matatizo mawili muhimu na idadi ya vifo milioni 5.4 iliyotolewa na IRC.

Anasema tatizo la kwanza wanaamini ni kwamba utafiti wa mwanzo ulofanywa wakati wa kipindi cha 1998 hadi 2001, ulifanyika bila ya kutumia utaratibu wa kisayansi unaofaa. Na tataizo la pili ni kwamba utafiti wao wa mwisho ulofanywa vizuri zaidi lakini ulitumia kiwango cha vifo kabla ya vita ambacho kilikua chini sana. Mack Anasema na unapochukulia kiwango cha chini kabla ya vita bila shaka utagundua kiwango cha juu sana ya idadi jumla ya vifo kutokana na vita.

Matokeo haya mepya yamezusha mabishano makubwa ndani ya Kongo baadhi wakisema idadi ya awali huwenda ikakubalika lakini wengine wakikubaliana na utafiti mpya kama anavyoeleza mbunge wa Kivu ya Kaskazini Ernest Kiaviro:

ninadhani idadi kamili haijulikani yani hakuna anaejua huyu amepigwa kwa risasi huyu amekufa ...hii idadi ya milioni tano sijui waipata wapi ninadhani walikwenda mbali mno sidhani imezidi milioni moja au mbili au tatu.

Bw Kiaviro anasema kwa vyovyote vile ni muhimu kuheshimu watu walofariki na ni vibaya kutoa idadi ambyo si ya kweli.

hatutasahau hata mtu moja amefariki lakini kama amefariki mtu mmoja tusiseme wamefariki kumi...ukiangalia hata kwa jamaa na majeshi walokua wanapigana huko hautaona idadi hizo za maajabu.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilitumia takwimu za IRC za vifo milioni 5.4 kuweza kuidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha wanajeshi elfu 20 huko DRC, ikiwa ni operesheni kubwa kabisa duniani inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Marc alisifu IRC kwa kusaidia katika kuleta mwangaza wa vita hivyo vya DRC kwa jumuia ya kimataifa, lakini alisema kundi lake lilikua na wasi wasi juu ya utaratibu ulotumiwa. Anasema ripoti yake haikosowi hata kidogo IRC bali inahisi kutumia utaratibu kama huu kufanya utafiti matokeo yake unapata takwimu zisizo sawa. Anasema kuna njia nyingine tofauti kuonesha athari za mzozo wa kibinadamu bila ya kutumia utaratibu kama huu unaozusha utata mkubwa.

Mack anasema kufuatana na utaratibu unaostahili, idadi ya vifo vya huko DRC huwenda ikashuka na kufikia laki 9.

Richard Brennan moja wapo wa walotayarisha ripoti ya IRC anasema ingawa kulikuwepo na vipingamizi katika kufanya utafiti wao katika mashariki ya Kongo iliyokumbwa na vita, haamini utaratibu huo unaweza kufutilia mbali matokeo yao.

Nikiripoti kutoka Makao Makuu huyu ni AWK wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM.