Skip to main content

Afisa wa UM anahimiza mkatati wa kupambana na uharamia Somalia

Afisa wa UM anahimiza mkatati wa kupambana na uharamia Somalia

Naibu Mjumbe Maalum wa UM kwa ajili ya Somalia Charles Petrie ametoa mwito wa kuwepo na mkakati thabiti na mpana wa kupambana na uharamia nje ya pwani ya Somalia, akieleza kwamba kuenea kwa tatizo hilo ni kutokana na kutumia mbinu ya kupambana nao baharini pekee yake.

Bw Petrie alikua anazungumza kwenye mkutano wa Kundi la Kimataifa la Ushauriano kwa ajili ya Somalia ambalo limeimarisha ushirikiano kati ya mashirika ya usafiri baharini na vikosi vya kijeshi katika eneo hilo. Mjumbe huyo maalum anasema licha ya juhudi hizo uharamia umeendelea kupanuka na kuenea mbali na ufukwe wa Somalia. Akiongezea kwamba tatizo limesababisha kuongezeka kwa gharama za usafiri kutokana na utaratibu wa usalama unaochukuliwa na mashirika ya usafiri wa meli.

Ripoti ya Katibu Mkuu iliyotolewa mwezi Novemba ilitoa mwito wa mkakati mpya wa pamoja utakaoimarisha uwezo wa serekali ya mpito ya Somalia na vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika kupambana na tatizo hilo katika nchi kavu, wakati huo huo kuimarisha mbinu za kupambana baharini.