Skip to main content

WHO yapongeza msaada wa dola bilioni 10 kutoka kwa taasisi ya Gates.

WHO yapongeza msaada wa dola bilioni 10 kutoka kwa taasisi ya Gates.

Shirika la Afya duniani limepongeza ahadi ya dola bilioni 10 ya msaada kutoka taasisi ya Bill na Melinda Gates ili kufanya utafiti, kutengeneza na kuwasilisha machanjo ya kuokoa maisha mnamo muongo moja ujao.

Mkurugenzi wa WHO Margaret Chan, alisema msaada wa taasisi ya Gates kwa ajili ya machanjo ni jambo ambalo halikuwahi kutokea, lakini hivi sasa anasema kunahitajika hatua nyingine kama hiyo ambayo haijawahi kutokea kusawazisha msaada huo. Alisema ni muhimu kabisa kwamba serekali na sekta za binafsi kuimarisha juhudi zao hivi sasa kutoa machanjo ya kuokoa maisha kwa watoto wanaohitaji zaidi.

Tangazo la Gates Foundation, lilitolewa Ijuma wakati wa mkutano wa Uchumi Duniani huko Davos Uswisi, na kutokea wakati wa kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa muungano wa kimataifa wa machanjo GAVI.

Tangu kuanzishwa mwaka 2000, ushirika huo wa kimataifa wa afya, umefanikiwa kuwafikia zaidi ya watoto milioni 257 walozaliwa na wale wasopata machanjo yanayohitajika.