Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM: watu milioni 1.1 wanahitaji makazi ya dharura Haiti.

UM: watu milioni 1.1 wanahitaji makazi ya dharura Haiti.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba kati ya watu laki tisa hadi milioni 1.1 wanahitaji msaada wa makazi ya dharura huko Haiti, wengi wao katika mji mkuu wa Port au Prince.

Kwa wakati huu bila shaka tunafanya kila tuwezalo kugawa plastiki za kutosha za kutengeneza hema kwa sababu kuna mahitaji makubwa, lakini wakati huo huo tuna mkakati wa kujenga hifadhi za kudumu. Ni kazi yenye utata mkubwa kwani tunafahamu kujenga hema haitokua suluhisho muafaka ukichukulia kwamba msimu wa mvua unakaribia, hivyo unahitaji majengo ya kudumu.

IOM inasema kwa upande mwengine imeanza mpango wa kugawa chakula kwa ajili ya kufanya kazi ili kusaidia kuondowa vifusi hasa katika mji mkuu wa Port au Prince.

Kwa upande wake idara ya huduma za dharura ya umoja wa mataifa OCHA inaeleza kwamba imeshapokea asili mia 77 ya fedha ilizoomba kwa ajili ya Haiti, yaani imepokea dola milioni 443 kati ya milioni 575 zilizohitajika. Idara hiyo imeeleza kwamba kazi ya kutathmini hali baada ya maafa itaanza hapo Febuari 8 ili kuweza kufahamu mahitaji ya kuikarabati nchi na kuwasilisha kwa mkutano wa wafadhili baadae mwezi Marchi hapa mjini New York.

Maji inabaki kua tatizo na UNICEF imeimarisha kazi za kutoa maji ili kuepusha uwezekano wa kuzuka magonjwa ya kuambukiza. Timu za watalamu wa afya za Shirika la Afya Duniani WHO, zinaripoti kuongezeka kwa kesi za kuharisha mnamo siku mbli zilizopita. Vile vile kuna ripoti zakuwepo na na ugonjwa wa pepodunda na surua na kusababisha wasiwasi miongoni mwa watalamu wa WHO.