UM: zaidi ya ajali asili 3 800 zilitokea muongo ulopita

28 Januari 2010

Idara ya Umoja wa Mataifa ya kujaribu kupunguza maafa imeeleza kwamba mnamo muongo uliyopita kumekuwepo na ajali asili 3 800 zilizosababisha vifo vya watu 780 000. Idara hiyo inakadiria ajali asili hizo zimesababisha uharibifu wa mali wa kiasi cha dola bilioni 960.

Mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya kupunguza hatari za maafa Margareta Wahlstrom amesema asili mia 60 ya vifo vilivyotokana na ajali asili vimesababishwa na mitetemeko ya ardhi. Alisema, tetemeko la ardhi linabaki kua kitisho kikubwa kwa mamilioni ya watu kote duniani kwani miji mikubwa minane yenye wakazi wengi duniani inapatikana katika maeneo ya mitetemeko ya ardhi. Maafa makubwa na mabaya zaidi ni Tsunami ya 2004 ambapo watu laki 2 na elfu 26 walifariki. Asia ndilo bara liliopoteza takriba asili mia 85 ya maisha ya binadamu kutokana na ajali asili mnamo muongo ulopita.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter