Ban: Msaada wa Kimataifa kwa Afghanistan usiwe kwa ajili ya usalama pekee

Ban: Msaada wa Kimataifa kwa Afghanistan usiwe kwa ajili ya usalama pekee

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, alitoa mwito kuwepo na mkakati wa kisiasa wenye mpangilo ili kuisaidia Afghanistan katika kutafuta amani, usalama na maendeleo, akieleza kwamba, changamoto za nchi hiyo haziwezi kutanzuliwa kwa njia ya kijeshi pekee.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan huko London, bw Ban alisema, lazima watu watambuwe kwamba, wakati usalama ni jambo muhimu kabisa katika mkakati wa mpito, lakini haijabidi liwe suala kuu na pekee la kuzingatiwa. Mkutano huo uloandaliwa kwa pamoja kati ya Bw Ban, Rais Hamid Karzai wa Afghanistan na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ulihudhuriwa na mataifa 70 kujadili njia za kuisaidia Afghanistan kuendeleza maendeleo yake baada ya uchaguzi wa mwaka jana, ambapo rais Karzai alipata ushindi wa muhula wa pili. Bw Ban alisema mkutano huo unatoa nafasi kuangalia mbele na kujadili upya ushirikiano kati ya Afghanistan na jumuia ya kimataifa na washirika wake, ushirikiano utakao kua chini ya misingi ya kuimarisha utawala na uwongozi wa Afghanistan, kuheshimu haki za binadamu, na kukidhi mahitaji msingi ya wananchi wa Afghanistan. Aliongeza kusema kwamba, licha ya kuongezeka matatizo ya kiusalama, afisi ya Umoja wa Mataifa huko Afghanistan, pamoja na washirika wa Umoja wa Mataifa wataendelea na nia ya kusaidia kwa muda unaohitajika, malengo ya wa-Afghan kuweza kufikia amani na ustawi.