Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unashiriki katika mkutano wa kimataifa juu ya Yemen

UM unashiriki katika mkutano wa kimataifa juu ya Yemen

Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa ataongoza ujumbe kushiriki katika mkutano wa mawaziri wa kimataifa uloanza mjini London siku ya Jumatano juu ya hali huko Yemen, wakati wasi wasi unaongezeka kuhusiana na kuzidi kwa ushawishi wa al-Qaida na makundi mengine yenye itikadi kali katika taifa hilo la Kiarabu.

Naibu Katibu Mkuu kwa ajili ya masuala ya Kisiasa B. Lynn Pascoe ni miongoni ma wajumbe wa UM wanaoshiriki kwenye mkutano ambao utajadili pia juu ya masuala ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za dharura kwa taifa hilo.

Wazir Mkuu wa Uingereza Gordon Brown alitayarisha mkutano huo wa siku moja wenye lengo la kuwakusanya pamoja maafisa wa serekali ya Yemen, UM na Jumuia ya Kimataifa kuamua jinsi wanavyoweza kwa pamoja kubakiliana na changamoto zinazoikabili Yemen, ikiwa ni pamoja na kitisho cha ugaidi.

Maafisa wa vyeo vya juu wa UM pamoja na katibu mkuu wameeleza wasi wasi wao katika miezi ya hivi karibuni juu ya hali ya huduma za dharura katika eneo la kaskazini magharibi ya nchi hiyo ambako mapigano kati ya majeshi ya serekali na waasi yamewalazimisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao.