Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa mataifa yanayoendelea

Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa mataifa yanayoendelea

Mkuu wa Idara ya kimataifa ya UM kwa ajili ya maendeleo ya kilimo, IFAD, anasema kilimo ndiyo inasukuma mbele ukuwaji wa uchumi wa mataifa yanoendelea kabla ya kuanza kwa mkutano wa wiki moja wa jopo la uchumi duniani huko Davos Uswisi.

Akihudhuria mkutano huo wa wafanyabiashara wa dunia na viongozi wa kisiasa, Bw Kanayo F Nwanze anatazamia kua sauti ya wakulima wadogo wa Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.

Mada ya mkutano huo wa kila mwaka utakaoanza Jumatano ni, "Kuimarisha hali ya dunia: Fikiria upya, kupanga upya, kujenga upya." Bw Nwanze alieleza kwamba watu wameanza kutambua kwamba wakulima wadogo na jamii za mashambani ni viungo muhimu katika kupatikana suluhisho kwa changamoto zinazojitokeza na ukosefu wa usalama wa chakula na umaskini.

Rais wa IFAD alisema, Kilimo, bila ya kujali ukubwa wa shamba, huzalisha biashara, na kila mjasirimali ikiwa ni mkulima mdogo au mkulima mkubwa wa biashara, wanacho kihitaji ni kupata fedha, na hivyo anasema ni jukumu lao kumbadilisha mkulima mdogo kua mfanya bishara mdogo.