Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM amelaani shambulio la bomu Mogadishu

Mjumbe wa UM amelaani shambulio la bomu Mogadishu

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu huko Somalia amelaani shambulio la bomu lililosababisha maafa siku ya Jumatatu katika mji mkuu wa Mogadishu, muda mfupi tu baada ya kuutembelea mji huo kwa mazungumzo na wakuu wa serekali.

Ahmedou Ould-Abdalah, alisema shambulio hilo halitowazuia maafisa wa kimataifa kuitembelea Mogadishu wala haitozuia serekali ya mpito ya nchi hiyo TFG, kuendelea na kazi zake.

Ripoti za vyombo vya habari zinaeleza mtu mmoja aliulia kutokana na shambulio dhidi ya zahanati inayoendeshwa na afisi ya walinda amani wa AU huko Somalia AMISOM. Mapema Ijumatatu Bw Ould-Abdallah alifuatana na Bw Ramtane Lamamra, Kamishna wa Amani na Usalama wa AU, pamoja na Mjumbe Maalum wa AU huko Somalia Boubacar Diara kwa mazungumzo na viongozi wa TFG.

Vipau mbele vya serekali na maendeleo ya hivi karibuni ya miundo mbinu mjini Mogadishu ilichukua nafasi kubwa katika mazungumzo yao iliyohudhuriwa na rais wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed.