Skip to main content

UNHCR: Operesheni za kijeshi na uhalifu zinasababisha wimbi jipya la wakimbizi

UNHCR: Operesheni za kijeshi na uhalifu zinasababisha wimbi jipya la wakimbizi

Idara inayowahudumia Wakimbizi ya UM, UNHCR inasema kuendelea kwa operesheni za kijeshi dhidi ya wapiganaji wa kihutu na makundi ya wahalifu wenye silaha katika jimbo linalokumbwa na ghasia la Kivu ya Kaskazini huko DRC kumesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao mnamo miezi miwili ilyiopita.

Tangu Disemba mwaka jana, UNHCR imewandikisha zaidi ya watu wepya 15 500 walokimbia makazi yao na kufika katika vituo vinavyoendeshwa na UNHCR ili kutafuta hifadhi na usalama. Kufuatana na watu wanaokimbia hali ni ngumu na hakuna usalama katika vijiji vyao sehemu za magharibi za Kivu ya Kaskazini.