Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Kimataifa juu ya Haiti unaahidi kujihusisha kwa miaka 10

Mkutano wa Kimataifa juu ya Haiti unaahidi kujihusisha kwa miaka 10

Mkutano wa kimataifa ulofanyika Montreal kujadili huduma kwa Haiti iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi umethibitish haja ya kujihusisha kimaendeleo na kuikarabati taifa hilo la Caribbean kwa angalao miaka kumi ijayo.

Katika taarifa ya mwenyekiti iliyoidhinishwa na mkutano huo, wajumbe walikubaliana juu ya misingi sita itakayo ongoza juhudi zao za pamoja kuelekea maendeleo na kuikarabati Haiti, kama vile kusimama bega kwa bega na Haiti kwa muda mrefu, kuheshimu uhuru wa Haiti, na kuratibu juhudi zao zote kupitia Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo, kwa muangalio wa ukubwa wa kazi za kukarabati, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton alitangaza kwamba Marekani itaandaa mkutano wa wafadhili mwezi Machi, utakaofanyika kwenye makao makuu ya UM . Alisema wafadhili wakuu wakiongozwa na Marekani, Canada, Brazil, Ufaransa na Umoja wa Ulaya wanajaribu mbinu mpya ya kutathmini mahitaji kabla ya kupanga na hapo tena kuchangisha fedha zinazohitajika.