Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM: Kucheleweshwa uchaguzi wa Afghan kutahakikisha matayarisho bora.

UM: Kucheleweshwa uchaguzi wa Afghan kutahakikisha matayarisho bora.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu kwa ajili ya Afghanistan Kai Eide, amepongeza uwamuzi wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa bunge kwa miezi minne, akisema hatua hiyo itawapatia maafisa wa uchaguzi nafasi zaidi ya kutayarisha uchaguzi huo.

Tume huru ya uchaguzi IEC ilitangaza mjini Kabul mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba itachelewesha uchaguzi hadi Septemba 18, ikieleza matatizo ya kifedha na usalama kua sababu za kuchukua hatua hiyo. Afisi ya mjumbe maalum nchini Afghanistan ilitoa taarifa ikieleza kwamba ingelikua vigumu sana kwa uchaguzi kufanyika kama ulivyopangwa, na nafasi hii itawawezesha pia kuimarisha utaratibu wote kutokana na mafunzo yaliyopatikana na uchaguzi wa rais na mabaraza ya majimbo 2009. Maafisa waligundua wizi wa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais. Kwa upande mwngine siku ya Alhamisi mkutano wa kimataifa wa wafadhili utafanyika kujadili njia za kuendelea mbele na maeneleo ya Afghanistan.