Mkuu mpya wa afisi ya UNAMID awasili Darfur

25 Januari 2010

Mkuu mpya wa afisi ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMIND, Profesa Ibrahim Gambari aliwasili mjini El Fasher, Darfur Jumatatu, na kukutana na maafisa wa makao makuu na kukagua gwaride la walinda amani katika jimbo hilo.

Akizungumza na watumishi wa AU na UM Gambari alitoa shukurani kwa kazi wanazofanya kwa niaba ya jumuia ya Kiamtaifa, akisema jukumu lake ni kuongoza kazi za afisi hiyo kuweza kutekleza wajibu wake kwa haraka iwezekanavyo. Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu alikutana pia na gavana wa jimbo la Darfur ya Kaskazini Ousman Yousiff, na kumshukuru kwa ushirikiano wake na kuhakikisha kuwepo na usalama.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter