Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA inasema hali ya usalama Haiti ni tulivu

OCHA inasema hali ya usalama Haiti ni tulivu

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura OCHA inasema hali katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince imebaki kua tulivu, ingawa kumekuwepo na matukio ya wizi wa ngawira na ghasia katika baadhi ya maeneo.

Kuna ripoti za watu wanaoendelea kuuhama mji mkuu kuelekea maeneo ambayo hayakuathirika. Kazi katika uwanja wa ndege zinaendelea vizuri kukiwepo na karibu ndege 150 zinazotua kila siku. Barabara kuelekea Jamhuri ya Dominica imebaki kua njia muhimu nzuri yakuwasilisha mizigo. UM umekodisha malori 21kutoka Dominica ili kusafirisha mafuta kila siku ya pili kutoka mji mkuu wa Santo Domingo hadi Port-au-Prince. Mwito wa msaada umeweza kufikia asili mia 36 ya dola milioni 575 zilizoombwa